Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amekabidhi pikipiki pikipiki mia moja kwa Umoja wa Madereva Mbeya , Chunya na Kyela(MBETUKYE) lengo ni kuwawezesha kiuchumi wanachama hao.
Mwenyekiti wa MBETUKYE George Mwakejela ameshukuru kupokea mkopo huo wenye riba nafuu ambapo pikipiki hizo zitawasaidia kuwakwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Dkt Tulia amewapongeza MBETUKYE kwa mshikamano wao hata kuwawezesha kupata mkopo huo.
Aidha amechukua fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoelekeza miradi mbalimbali Jijini Mbeya ukiwepo mradi wa barabara wa TACTICS kilometa 22 na barabara Kuu na ile ya mchepuo sanjari na mradi mkubwa wa maji Kiwira.
Dkt Tulia Ackson amewahakikishia wananchi wote Jijini Mbeya kuwa changamoto ya maji katika mitaa yote itakwisha hivi punde.
Katika hatua nyingine ameahidi kukaa pamoja na wamiliki wa mabasi ili kuhakikisha mikataba ya Madereva inarekebishwa.
Pamoja na hayo amewataka madereva kutoshusha abiria nje ya Kituo cha nane nane.
Amehitimisha kwa kuwataka wananchi kuwa walinzi kwa miundombinu mbinu ya barabara.